Dar Es Salaam. Mahakama ya kuwahukumu Wanyarwanda Arusha imekubwa na shutuma kadha.
14 Septemba 2005Mahakama maalum iliyoundwa kuwahukumu wale waliopanga na kutekeleza mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994, imesema leo kuwa imeamuru kuunda tume ya uchunguzi kuhusu madai ya ukiukaji wa utaratibu uliotumika kumwajiri afisa mmoja mwaandamizi.
Licha ya bajeti ya mamilioni ya dola , mahakama hiyo imekumbwa na madai kadha ya kutoweza kufanyakazi kwa ufanisi na iko katika nafasi ngumu kuweza kufikia lengo la kumaliza kazi ya kuwahukumu watuhumiwa wote ifikapo 2008.
Mahakama ya kimataifa ya kuwahukumu wahalifu wa Rwanda ICTR, iliyoko katika mji wa kaskazini nchini Tanzania wa Arusha iliundwa kuwahukumu wale waliohusika na mauaji ya Watutsi 800,000 pamoja na Wahutu waliokuwa na msimamo wa kati waliouwawa na Wahutu wenye msimamo mkali.