1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Dira yaifikisha serikali mahkamani

17 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFrY
Wachapishaji wa gazeti la kujitegemea visiwani Zanzibar Tanzania wamekwenda mahkamani kujaribu kutenguwa kupigwa marufuku na serikali kwa gazeti hilo la kila wiki hapo mwezi uliopita. Mrajisi wa Mahkama Kuu Zanzibar Mbarouk Salum Mbarouk ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwa njia ya simu kutoka Zanzibar kwamba wamepokea ombi hilo na kwamba wanalifanyia kazi ili kesi hiyo ianze kwa haraka Mbarouk amesema katika ombi hilo lililowasilishwa mahkamani hapo Jumatatu chini ya hati ya dharura wachapishaji wa Dira wameitaka mahkama kutenguwa agizo la waziri ya kulipiga marufuku gazeti hilo. Waziri wa Nchi kwa masuala ya habari wa Zanzibar Salum Juma Othman mwezi uliopita alilipiga marufuku gazeti hilo kwa kusema kwamba kurepoti kwake kunakiuka maadili ya uandishi. Siku chache baadae Mkurugenzi wa Idara ya Habari Zanzibar Enzi Talib Aboud alifuta leseni ya gazeti hilo. Mahkama ya Zanzibar mwezi wa Oktoba uliopita uliamuru wachapishaji wa gazeti hilo la Dira kulipa fidia ya dola 660,000 kutokana na makala za kashfa dhidi ya mtoto wa kiume na wa kike wa Rais Aman Abeid Karume wa Zanzibar.