Dar Es Salaam. Clinton azuru Tanzania, katika uhamasishaji dhidi ya ukimwi.
20 Julai 2005Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo ambapo anatarajiwa kuzindua mpango mpya wa kupambana na ukimwi ikiwa ni nchi ya nne kati ya nchi sita za Afrika anazozitembelea, ili kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo mbaya.
Bwana Clinton anatarajiwa kuwasili mjini Dar Es Salaam mchana huu akitokea Afrika kusini na atazindua mpango huo pamoja na rais wa Tanzania Benjamin Mkapa mpango ambao ni wa kuwaandikisha na kuwapa mafunzo wafanyakazi wa sekta ya afya watakaofanyakazi katika nyanja ya utunzaji wa wagonjwa wa ukimwi pamoja na utawala katika maeneo ya vijijini nchini Tanzania.
Mpango wa taifa wa rais Benjamin Mkapa wa kupambana na ukimwi, ambao utapata fedha kutoka katika mfuko wa kutoa misaada wa rais huyo wa zamani wa Marekani Bill Clinton , unapanga kuwapa mafunzo na kuwapeleka katika maeneo ya vijijini kiasi cha wafanyakazi 30 kwa mwaka.