1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dar Es Salaam. Baraza la usalama lasifu hatua za amani.

11 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJe

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limetoa sifa kwa hali ya usalama inayoendelea kuimarika katika eneo tete la maziwa makuu barani Afrika, jana , ikiimwagia sifa Tanzania kwa jukumu ililochukua katika hatua za kuleta amani nchini Burundi.

Balozi wa Ufaransa katika umoja wa mataifa Jean-Marc de la Sabliere ambaye anauogoza ujumbe huo wa baraza la usalama amesema kuwa ni dhahiri kuwa hali sasa inaimarika.

Hatua za mpito nchini Burundi sasa zimekamilika. Uchaguzi utafanyika nchini Congo na uhusiano kati ya mataifa licha ya kuwa hauko imara sana , lakini ni mzuri kiasi , Sabliere amewaambia waandishi wa habari mjini Dar Es Salaam ikiwa ni kituo cha mwisho katika ziara yao ya mataifa ya maziwa makuu.