DAMASKUS: Marekani yaitaka Syria iondoshe majeshi yake nchini Lebanon
2 Machi 2005Kwa mara nyingine tena, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleeza Rice, ameikemea Syria. Akizungumza na shirika la matangazo ya televisheni la Uingereza alisema, siasa za Syria na msimamo wake, unachelewesha maisha mazuri ya kidemokrasia kwa wananchi wa Mashariki ya kati.
Bi. Condoleeza Rice ameitaka pia Syria iondoshe wanajeshi wake elfu-14 nchini Lebanon.
Russia nayo imeikata Syria kuondosha majeshi yake nchini Libanon: Serikali ya Syria lazima itekeleze azimio la Umoja wa Mataifa la mwezi wa Septemba, amesema msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Russia, Alexander Jakowenko.
Rais wa syria, BASCHAR EL ASSAD, aliliambia gazeti Marekani, TIME kuwa, nchi yake itaondosha majeshi yake nchini Lebanon katika kipindi cha miezi michache ijayo. Ahadi kama hizi ziliwahi kutolewa na kiongozi huyu bila ya kuzitekeleza.