1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Vikosi kuondoshwa Lebanon

13 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFXU

Syria imeahidi kuwa hadi mwisho wa mwezi Machi itaondosha theluthi moja ya vikosi vyake kutoka Lebanon,hiyo ikiwa awamu ya mwanzo ya mpango wa kuyaondosha majeshi yote.Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Trje Roed Larsen amepewa ahadi hiyo baada ya kuwa na mazungumzo pamoja na rais Bashar al-Assad mjini Damascus siku ya jumamosi.Hii leo Larsen anakutana na maafisa wa Lebanon.Tume ya pamoja ya maafisa wa kijeshi wa Lebanon na Syria itakutana mwezi April kupanga tarehe ya kuondoshwa vikosi vya mwisho.Syria imekuwa na vikosi vyake nchini Lebanon tangu miaka 29,lakini shinikizo la kuviondosha vikosi vyake lilizidi baada ya kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik al-Hariri mwezi wa Februari.Damascus inalaumiwa na wananchi wengi wa Lebanon kuhusika na mauaji ya Hariri.