DAMASCUS: Syria yatishia kuufunga mpaka na Lebanon
24 Agosti 2006Matangazo
Syria imesema itaufunga mpaka wake na Lebanon ikiwa Umoja wa Mataifa utawapeleka wanajeshi wa kulinda amani kusini mwa Lebanon, kama sehemu ya juhudi za kutekeleza azimio la kusitisha mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Syria, Walid Al-Moualem alitoa kitisho hicho alipokutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Finlad, Erkki Tuomioja, mjini Helsinki hapo jana.
Hatua hiyo itakata mawasiliano kati ya Lebanon na ulimwengu wote, kwani jirani wake mwingine ni Israel, taifa ambalo hailitambui, na bado Israel imeizingira Lebanon angani na baharini.
Rais wa Syria, Bashar al Assad, amesema ataichukulia hatua ya kupelekwa kikosi cha kimataifa kwenye mpaka wa Lebanon na Syria kuwa kitendo cha kikatili.