1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS-Syria yatangaza kumaliza kazi ya kuwaondosha wanajeshi wake kutoka Lebano kabla ya uchaguzi wa mwezi Mei nchini Lebanon

30 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFS7

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria,Farouq al-Shara amesema kwa mara ya kwanza nchi yake itaviondoa vikosi vyake vyote kutoka Lebanon kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Lebanon.

Waziri huyo ameyaeleza hayo katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bwana Kofi Annan.

Barua hiyo ya Bwana al-Shara inaeleza kuwa Syria imekwishawaondosha wanajeshi wake 10,000 kati ya 40,000 kutoka Lebanon.Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa kazi ya kuwaondoa wanajeshi wote wa Syria itakamilika kabla ya uchaguzi utakaofanyika mwezi wa Mei.

Shinikizo kwa Syria kuondosha wanajeshi wake kutoka Lebanon,lilishika kasi mwezi uliopita baada yakuuawa Waziri Mkuu wa zamani wa Lebani,Rafik Hariri,ambapo Syria imeshutumiwa kuhusika na mauaji hayo.