Damascus. Syria yasema Lebanon inapaswa kujiunga nayo katika mazungumzo na Israel.
13 Julai 2005Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Syria amesema katika matamshi yaliyochapishwa leo kuwa nchi yake inataka Lebanon kujiunga nayo katika mazungumzo yeyote ya kuleta amani na Israel.
Waleed al-Mualem aliyaambia magazeti ya Syria ya Al Thawra na Kuwait al –Anbaa katika mahojiano ya pamoja kuwa msimamo wa Syria na Lebanon haujatofautiana na sababu zinafahamika wazi.
Bwana Mualem ameeleza matumaini yake kuwa Lebanon , ambayo hivi sasa haina tena majeshi ya Syria kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 30, haitatia saini makubaliano tofauti ya amani na Israel chini ya ushawishi wa Marekani.
Lebanon inauchaguzi hivi sasa , ama ielekee upande wa Marekani hii ikiwa na maana upande wa Israel, ikiwa ni uwezekano mdogo sana kutokana na kile kinachofahamika kuhusu watu wa Lebanon, ama upande wa Waarabu. Syria itakuwa daraja amesema kwa Lebanon kuelekea upande wa Waarabu.