DAMASCUS: Syria yaitikia kuondoka Lebanon
7 Machi 2005Viongozi wa Syria na Lebanon Emile Lehoud na Bashar Al assad wamefikia uamuzi wa tarehe ya mwisho ya kuondoka kwa majeshi ya Syria nchini Lebanon.Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wa Damascus,Maafisa wamesema majeshi hayo yataondoka ifikiapo mwisho wa mwezi marchi.
Hata hivyo jumuiya ya Ulaya ikiwa ni pamoja na Ufaransa Ujerumani na Marekani imeitaka Syria kuondosha mara moja majeshi yake nchini Lebanon. Mjini Beirut maandamano ya wafuasi wa upinzani yanaendelea huku chama cha Hezzbollah kikitangaza mandamano makubwa hapo kesho yakupinga mpango wa kuyaondosha majeshi ya Syria nchini Lebanon.
Wakati huo huo rais wa Lebanon ametangaza kwamba atafanya mazungumzo na wabunge siku ya jumatano juu ya kumchagua waziri mkuu atakayechukua nafasi ya waziri mkuu aliyejiuzulu.