DAMASCUS :Syria kuondowa vikosi Lebanon tarehe 30 April
3 Aprili 2005Matangazo
Syria itaondowa wanajeshi na majasusi wake wote kutoka Lebanon ifikapo tarehe 30 mwezi wa April.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari wa pamoja na Waziri wa mambo ya nje wa Syria Farouq al Shara mjumbe wa Umoja wa Mataifa Terje Roed Larsen amesema Shara amemhakikishia kwamba wanajeshi, zana za kijeshi na majasusi wote wa Syria watakuwa wamekwishaondolewa ifikapo tarehe 30 mwezi wa April.Amesema Syria imekubali kwa kutegemeana na serikali ya Lebanon kwa Umoja wa Mataifa kutuma timu ya kuyakinisha kuondolewa kwa vikosi hivyo.
Roed Larsen alikuwa akizungumza kufuatia mazungumzo yake na Rais Bashar al Assad.