1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria kuondoa majeshi yake kutoka Lebanon.

25 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFb4

Serikali ya Syria imesema kuwa itaanza kuondoa wanajeshi wake wapatao alfu 14 kutoka Lebanon na kuyapeleka mashariki mwa nchi yake kufuatia makubaliano ya mika 16 iliyopita.

Hatua hii ni kutokana na maandamano na upinzani mkubwa kwa Syria baada ya kuuwawa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik al hariri.

Serikali ya Syria inapinga kuundwa kwa tume ya kimataifa ya uchunguzi kufuatia kifo cha Hariri lakini imekubali kushirikiana na ujumbe wa umoja wa mataifa.