1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Rais wa Syria awashambulia viongozi wa Lebanon

10 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJj

Rais wa Syria, Bashar al-Assad amewashambulia maofisa wa Lebanon na akatangaza kwamba nchi yake haikuhusika katika mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon, Rafik Hariri.

Assad amesema maadui wanaopanga njama dhidi ya Syria hawatafaulu na kizazi cha sasa kitadhihirisha kwamba Syria ni taifa imara kama vizazi vilivyopita. Ameongeza kusema Syria haitaki kuingiliwa mambo yake ya ndani na wala haitokubali shinikizo la kimataifa.

Rais Assad amesema mchunguzi wa Ujerumani, Detlev Mehlism, amekataa mwaliko wa kwenda Damascus kusaini mkataba wa ushirikiano. Hata hivyo ameahidi kwamba serikali ya Damascus itashirikiana na timu ya wachunguzi wa umoja wa mataifa.

Maelfu ya wanafunzi waliokuwa wamebeba bendera za Syria, walimshangilia rais Assad alipokuwa akihutubia katika chuo kikuu cha Damascus.