DAMASCUS: Marais wa Syria na Lebanon wakutana
7 Machi 2005Marais wa Syria na Lebanon wanakutana leo kwa mazungumzo yakuidhinisha mpango wa Syria wa kuyaondosha majeshi yake kutoka Lebanon.
Rais wa Syria Bashar Al-Assad amependekeza majeshi yake yaondoke katika awamu mbili ijapokuwa Marekani imesisitiza kwamba Syria iondoke Lebanon kabla ya uchaguzi mnamo mwezi wa Mei.
Hata hivyo waziri wa Ulinzi wa Lebanon amesema mpango wa kuondoka kwa majeshi ya Syria utaanza punde baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya Damascus kati ya Marais Bashar Al Assad na Emile Lahaoud.
Kutokana na kuhinikizwa na jumuiya ya kimataifa rais wa Syria Bashar Al Assad alitangaza hatua ya kuondosha majeshi ya nchi yake kutoka lebanon bila mpango kamili.
Wakati huo huo chama cha Hezbollah kimeitisha maandamano jumaane kupinga mpango huo na kimetahadharisha juu ya vurumai inayoweza kutokea nchini Lebanon baada ya majeshi ya Syria kuondoka.