DAMASCUS: Majeshi ya Syria kuihama Lebanon mwishoni mwa April.
4 Aprili 2005Matangazo
Syria imeahidi kuyaondosha majeshi yake yote kutoka Lebanon kufikia mwisho wa mwezi wa april na kutaka umoja wa mataifa uwepo kushuhudia tendo hili.
Hayo ni kwa mujibu wa muwakilishi wa umoja wa mataifa Terje Roed Larsen ambaye aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na rais wa Syria Bashar al Assad mjini Damascus.
Kuondoshwa kwa majeshi ya Syria nchini Lebanon baada ya kuwepo huko kwa miaka 30 iliyopita kunafuatia shinikizo kutoka jamii ya kimataifa baada ya kuuwawa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik hariri mwezi februari.