1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damascus. Maafisa wa Syria watakiwa kufanyiwa mahojiano nchini Lebanon.

13 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIl

Kiongozi wa uchunguzi wa umoja wa mataifa kuhusu kifo cha waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri anasisitiza kuwahoji maafisa wa Syria nchini Lebanon , akipuuzia pendekezo la Syria la kutaka watu hao wafanyiwe mahojiano sehemu nyingine.

Afisa wa wizara ya mambo ya kigeni ya Syria ambaye hakutaka jina lake kutajwa , amesema kuwa mshauri wa masuala ya kisheria wa wizara hiyo Riad al- Daoudi amekutana katika mji mkuu wa Lebanon wiki iliyopita na Detlev Mehlis, ambaye anajaribu kuwatafuta wauawaji wa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.

Lakini afisa huyo amesema kuwa mwendesha mashtaka huyo kutoka Ujerumani amekataa kujadili wasi wasi wa Syria kuhusu ni mahala gani maafisa wake wakahojiwe na amepuuzia pendekezo la pili .

Kikosi cha Mehlis kinataka kuwahoji maafisa hao wa Syria , ambao wanasemekana na duru za kisiasa za Lebanon kuwa ni pamoja na shemeji yake rais Bashar al – Assad katika makao yake makuu karibu na Beirut.