CRAWFORD: Bush ataka msaada zaidi kutoka NATO
22 Mei 2007Matangazo
Rais wa Marekani George W.Bush amesema,anapanga kuwashinikiza wanachama wa Shirika la kujihami la magharibi-NATO kugawana mzigo nchini Afghanistan, huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka.Bush alitamka hayo,baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa NATO,Jaap de Hoop Scheffer katika shamba lake mjini Crawford,Texas nchini Marekani.