1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cotonou: Vikosi vya uokozi vinaendelea kuwasaka maiti...

26 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFp0

au watu waliosalimika na ajali ya ndege katika fukwe za mjini Cotonou nchini Benin.Ndege hiyo chapa Boeng 727 imeangukia baharaini ilipokua njiani kuelekea Beyrouth nchini Libnan.Kwa mujibu wa waziri wa afya wa Benin Céline Segnon watu wasipoungua 111 wameuwawa na wengine 22 kunusurika na ajali hiyo.Wengi wa wahanga wa ajali hiyo ni raia wa Libnan waliokua wakirejea nyumbani kwa sherehe za mwaka mpya.Ndege hiyo ilitokea Conacry nchini Guinee,na kutua pia Freetown nchini Sierra Leone na baadae Cotonou.Ndege hiyo ya shirika la usafiri barani Afrika UTA-inaamilikiwa na raia wawili wa Libnan. Utafiti unafanywa kujuaa chanzo halisi cha ajali hiyo. Vibweta viwili vyeusi vinavyonasa mawasiliano ndani ya ndege vimeshaopolewa.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Libnan Jean Obeid akifuatana na ujumbe muhimu wa nchi yake wamewasili Cotonou kusimamia shughuli za kuwarejesha nyumbani wahanga wa ajali hiyo.Jamii kubwa ya walibnan inaishi katika nchi za Afrika magharibi na wengi wao ni wafanyabiashara.