Cote d'Ivoire yaanza mazungumzo na wanajeshi
9 Januari 2017Matangazo
Donwahi amesema ametumwa na rais kukutana na wanajeshi hao na kuwasikiliza kwa lengo la kupata suluhisho. Mgomo wa wanajeshi ulioanzia mjini Bouake jana Ijumaa ulienea hadi mji wa Man ulioko magharibi mwa Cote d'Ivoire.
Serikali imesema kuwa wanajeshi hao wanataka kuongezwa mshahara, na kuharakishwa utaratibu wa kuwapandisha vyeo. Ingawa rais Alassane Ouattara amekwenda nchini Ghana katika sherehe za kumwapisha rais mpya, anatarajiwa kurejea nchini jioni. Kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kimeitishwa kujadili mgomo huo wa wanajeshi.
Mwaka 2014 serikali ya Cote d'ivoire ilitumia fedha kuwatuliza wanajeshi waliokuwa wamefanya mgomo kama huu mjini Bouake.