Corona yazuwia mkutano mkuu wa Borussia Dortmund 2020
8 Oktoba 2020Mkutano huo ulipangwa kufanyika Novemba 22 lakini rais wa Borussia Dortmund, Reinhard Rauball, amesema katika taarifa ya klabu hiyo kuwa kuwa na wanachama wengi iwezekanavyo katika tukio hilo hakuwezekani kutokana na vizuwizi, na mkutano kwa njia ya vidio hauwezekani pia katika mwaka 2020.
"Kukiwa na karibu wanachama 160,000 wa BVB, kwa bahati mbaya hakuna njia ya teknolojia ya kufanya mkutano kama huo kwa njia ya vidio katika hali ya inayokubalika," alisema.
"Binafsi nasikitika kwa hili, kwa kuwa mawasiliano ya moja kwa moja nanyi, wanachama wetu, ni muhimu sana kwetu."
Mkutano wa wadau wa Dortmund kwa wakati huu utafanyika kwa njia ya mtandao, Novemba 19, limesema gazeti la Kicker.