1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Conservative yamsimamisha mbunge kutokana na matamshi tata

Sylvia Mwehozi
25 Februari 2024

Chama tawala cha Uingereza cha Conservative kimemsimamisha mmoja wa wabunge wake Lee Anderson, baada ya kukataa kuomba radhi kwa kauli yake ya kibaguzi dhidi ya Meya wa London Sadiq Khan.

https://p.dw.com/p/4cr9v
England London | Lee Anderson
Mbunge wa Uingereza Lee Anderson kwa chama cha ConservativePicha: Yui Mok/empics/picture alliance

Chama tawala cha Uingereza cha Conservative kimemsimamisha mmoja wa wabunge wake Lee Anderson, baada ya kukataa kuomba radhi kwa kauli yake ya kibaguzi dhidi ya Meya wa London Sadiq Khan. Mbunge huyo wa Ashfield, alinukuliwa siku ya ijumaa akisema kuwa Meya Sadiq Khan anadhibitiwa na Waislamu.

Matamshi hayo tata yalilaaniwa sana na kutajwa kuwa ya ubaguzi wa rangi na chuki ya dhidi ya Uislamu na kuchochea shinikizo kwa Waziri Mkuu Rishi Sunak kuchukua hatua dhidi ya mbunge huyo.

Soma: Sunak ametuliza mivutano ndani ya Conservative?

Hayo yanajiri wakati matukio ya chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya Wayahudi yakiongezeka kwa kasi nchini Uingereza. Anderson, ambaye sasa atakaa kama mbunge huru bungeni, alisema Jumamosi kwamba anaelewa maoni yake yamemweka Sunak katika "hali ngumu" lakini hakuomba msamaha.