Congo yakanusha kukubali operesheni na jeshi la Uganda
30 Novemba 2021Matangazo
Congo imesisitiza kuwa nchi hizo mbili zinabadilishana tu taarifa za intelijensia.
Ripoti za kuwepo kwa kampeni hiyo ya pande zote za mpakani, ambazo zilithibitishwa na vyanzo viwili vya kidiplomasia, zimezusha wasiwasi miongoni mwa baadhi ya Wakongo, wanaokumbuka jukumu la Uganda katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomazilika mwaka wa 2003.
Msemaji wa serikali ya Congo Patrick Muyaya amesema majeshi ya nchi hizo mbili yamekuwa yakibadilishana habari kwa miezi mingi, na kuwa hakuna wanajeshi wa Uganda walioko nchini Congo kwa sasa.
Amesema kile serikali ilisema ni kuwa kutakuwa hatua za pamoja za kupambana na waasi na wala sio operesheni za pamoja.
Waasi hao wanatuhumiwa kufanya mashambulizi ya mabomu ya kujitoa muhanga mjini Kampala.