Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeukubali muswada wa kurekebisha sheria ya uchaguzi. Kikao kilichofanyika hapo jana pia kiliamua kuandaliwa mikutano mingine ili kuichunguza sheria hiyo kwa makini kabla ya kuanza kuitumia. Baadhi ya mapendekezo hayajashughulikiwa kwa sababu yanahitaji marekebisho ya katiba. Mengi zaidi na mwandishi wetu wa Kinshasa, Jean Noël Ba-Mweze.