1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Condoleezza Rice azuru Colombia

25 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cxc2

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, yumo nchini Colombia kwa mazungumzo kuhusu mikataba ya biashara huru.

Condoleezza Rice amesema Marekani inataka kuonyesha inamuunga mkono mmoja kati ya washirika wake wakubwa katikaneo hilo.

Kiongozi huyo amewasili Medellin akitokea mjini Davos nchini Uswisi ambako alihudhuria shehere za ufunguzi wa mkutano kuhusu uchumi.

Condoleezza Rice atakutana leo na rais wa Colombia, Alvaro Uribe,pamoja na kundi la wapiganaji wa zamani wa nchi hiyo, wakati wa ziara yake fupi mjini Medellin.

Meya wa mji huo amesema Condoleezza Rice alipendekeza kukutana na rais Uribe mjini Medellin, ambao ulikuwa zamani kituo cha ulanguzi wa dawa za kulevya, kama sehemu ya juhudi za ikulu ya Marekani kujaribu kulishawishi bunge la Marekani lipitishe mkataba wa biashara huru kati ya Marekani na Colombia.

Chama cha Democratic bungeni kinapinga mkataba huo kikisema rais Uribe hajafanya mengi kuzuia ukandamizaji wa vyama vya wafanyakazi.