Conakry:Viongozi wa wafanya kazi nchini Guinea wanakataa kufanya mazungumzo na serekali hadi amri ya kijeshi imeondoshwa nchini
18 Februari 2007Matangazo
Katika nchi ya Afrika Magharibi ya Guinea, viongozi wa vyama vya wafanya kazi wamekataa kufanya mazungumzo yenye nia ya kuikomesha michafuko hadi pale rais wa nchi hiyo, Lansana Conte, atakapoifuta sheria ya kijeshi katika nchi hiyo. Zaidi ya watu 100 wameuwawa katika michafuko ilioanza baada ya kuitishwa mgomo mkuu hapo Januari 10. Mashahidi na jumuiya za kupigania haki za binadamu zimelilaumu jeshi la nchi hiyo kwa kuwashambulia raia na kupora mali baada ya sheria ya hali ya hatari kutangazwa jumatatu iliopita.