1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY: Baraza jipya la mawaziri latangazwa nchini Guinea

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEY

Serikali mpya iliyotangazwa nchini Guinea imemaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.Baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na waziri mkuu Lansana Kouyaté limetimiza masharti makuu ya upinzani kwani halina hata waziri mmoja aliekuwepo katika serikali ya zamani ya Rais Conte.Kufuatia machafuko makali yaliyozuka nchini humo,Rais Conte aliechukua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 1984,alimteua Kouyaté kuwa waziri mkuu hapo mwezi wa Februari na akamkabidhi dhamana ya kuunda serikali mpya.