COLOMBO: Sri Lanka yapokea zaidi ya Euro Bilioni moja.
8 Aprili 2005Matangazo
Serikali ya Sri Lanka imetangaza kupokea zaidi Euro billioni moja katika mfuko wake wa janga la Tsunami lililotokea december 26 mwaka uliopita na kuwauwa watu 40,000 katika pwani ya Sri Lanka pekee.
Serikali ya Sri Lanka imesema kuwa fedha hizo zitatumika katika kujenga tena upya sehemu zilizo athirika na Tsunami.
Tayari mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo yameanza harakati za ujenzi wa mashule, na makaazi ya muda kwa familia zilizo athirika.
Inakisiwa kiasi cha Euro bilioni moja nukta tano huenda zikatumika kuijenga upya pwani ya Sri Lanka.