1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Clinton kuratibu misaada katika maeneo yalioathirika kwa Tsunami

29 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF8z

Rais wa zamani wa Marekani,Bill Clinton amewahimiza wanasiasa wa Sri Lanka washirikiane na waasi wa Tamil Tigers katika ujenzi mpya wa maeneo yalioathirika vibaya mwaka jana kwa Tsunami.Clinton amekwenda Sri Lanka kama sehemu ya ziara ya kuiona hali halisi ya eneo la Kusini na pia Kusini-mashariki mwa Asia,ili kuratibu misaada katika eneo hilo lililoteketezwa na mawimbi makubwa ya bahari.Clinton amesema analiunga mkono pendekezo lililotolewa na serikali ya Colombo na Tamil Tigers,kugawana misaada ya ujenzi mpya.Akaongezea kuwa ushirikiano huo utasaidia pia utaratibu wa amani.Desemba 26,takriban watu 31,000 waliuawa na Tsunami katika kisiwa cha Sri Lanka.