COLOGNE:Baba mtakatifu ahimiza masikilizano kati ya wakristo na wayahudi
19 Agosti 2005Kiongozi wa kanisa katoliki duniani baba mtakatifu Benedikt wa 16 hapa ujerumani amelaani mauaji ya kiholela yaliyofanywa na wanazi wakati wa vita vya pili vya dunia alipolitembelea hekalu la wayahudi mjini Kolon.
Kiongozi huyo pia amesisitiza haja ya kuwepo maelewano kati ya wakristo na wayahudi duniani.
Awali baba mtakatifu alikutana na rais wa shrikisho la jamhuri ya ujerumani Horst Kohler hapa mjini Bonn.
Mjini Kolon kiongozi huyo pia amekutana na viongozi wa dini mbali mbali ikiwemo wa dini ya kiislamu na wasiokuwa na dini.
Kilele cha Kongamano la vijana duniani kitafikiwa jumapili ijayo katika uwanja wa Marien Feld ambapo kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni ataongoza misa maalum mbele ya waumini vijana zaidi ya laki nane kutoka kila pembe ya dunia.