COLOGNE : Köhler ashutumu kiburi cha Ulaya dhidi ya Afrika
11 Juni 2007Mkutano wa Kanisa la Kilutheri nchini Ujerumani umemalizika kwa misa kubwa ya wazi mjini Cologne.
Takriban watu 100,000 walihudhuria mkutano huo wa siku tatu.
Kikao cha siku ya kwanza kiligusia masuala mbali mbali kuanzia utandawazi,mabadiliko ya hali ya hewa hadi umaskini. Rais Horst Köhler wa Ujerumani ameshutumu kile alichokielezea kuwa ni kiburi cha Ulaya dhidi ya mataifa ya Kiafrika.
Kadhalika rais huyo wa Ujerumani ambaye alishiriki kwenye kikao juu ya utandawazi na masuala kadhaa ya Ulaya pia alikuwa na haya ya kusema.
(O-TON Köhler)
Rais Kohler anasema michango ilioahidiwa kwa Afrika lazima itolewe na kwamba tayari kumejengwa imani lakini lazima wasisitize kwamba barani Afrika kunakuwepo na utawala bora,hakuna rushwa na kuendelezwa kwa vijana na kwamba Afrika yenyewe ijibunie sifa hizo nzuri.
Akiungana na kauli ya rais huyo Kansela Angela Merkel Ujerumani amesema Ulaya haipaswi kulazimisha kuweka ufumbuzi wa mtindo wa Ulaya kwa matatizo ya Afrika.