1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea Clinton na Trump washambuliana

10 Oktoba 2016

Wagombea urais wa Marekani Hillary Clinton na Donald Trump hawakupoteza muda katika mdahalo wao pili kabla ya kuanza kuzungumzia vidio iliyorekodiwa 2005 juu ya majadiliano yake ya uasharati kuhusu wanawake.

https://p.dw.com/p/2R3zT
US TV Debatte Trump vs Clinton
Picha: picture alliance/AP Photo/J. Locher

Wagombea hao wawili walikwepa kupeana mikono wakati wakielekea katika jukwaa la mdahalo la St.Lous, Missouri na ghafla wakaanza kushambuliana kwa maneneno makali.  Kuhusu vidio iliyosambazwa Ijumaa, bilonea wa New York, Trump alisikika kwa sauti kubwa akizungumzia vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake. Moja kati ya waendesha mjadala Anderson Cooper alimwambia "unajivunia kudhalilisha wanawake kingono" .

Kabla ya kubadili mada kuanza kuzungumzia mkakati wa kukabiliana na kundi la Dola la Kiislamu, Trump alijitetea "Hapana sikusema hivyo hata kidogo, nafikiri hukuelewa ilivyokuwa, haya yalikuwa mazungumzo ya mzaha, sijivunii jambo hilo, naomba msamaha kwa familia yangu, naomba msamaha kwa watu wa Marekani. Kwa hakika sioni fahari ya jambo hili."

Baadea akabidili mada akisema wanapaswa kujikita katika masuala muhimu ambapo akajigamba kulishinda kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu. Lakini muongoza mdahalo hakumwacha alimrudisha katika mada kwa kumohoji"umewahi kufanya mambo hayo?" Trump akajibu "Hapana, sijawahi."

Tangu Ijumaa iliyopita maafisa kadhaa mashuhuri wa chama chake cha Repulican, wakiwemo baadhi ya wabunge wa bunge la Marekani walijetenga na Trump kufuatia vidio hiyo iliyorekodiwa 2005. Wengi waliamua kutokumuunga mkono. 

Fimbo muhimu ya Clinton

US TV Debatte Trump vs Clinton
Hillary Clinton na Donald Trump katika mdahaloPicha: Reuters/R. Wilking

Kashfa hiyo ilikuwa fimbo muhimu kwa mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton ya kumchapia mpinzani wake. "Donald Trump ni tofauti, nilisema hivyo tangu Juni kwamba hafai kuwa rais na amiri jeshi mkuu. Na wengi kutoka Republican na Independent wamesema jambo hilo. Kile tulichokiona na kusikia Ijumaa, ilikuwa Donald anazungumzia wanawake. Anafikiri nini kuhusu wanawake, anafanya nini kwa wanawake na amesema vidio haiwakilishi namna alivyo lakini ni dhahiri kwa kila mtu aliyesikia kwamba inaonesha wazi jinsi alivyo"

Utafiti mpya wa maoni uliyotolea shirika la habari la ABC na taasisi ya kura ya maoni unaonesha muda mfupi kabla ya kuanza kwa mjadala huo unaonesha tangu kuanza kusambazwa kwa vidio ya kashfa ya Trump unasema asilimia 43 ya watu wanataka mgombea huyo ajiondoe katika kinyang'anyiro na 53 wanataka abakie.

Msimamo mpya kuhusu Waislamu

Katika mdahalo huu Trump ameondosha ile marufuku ya kudhibiti wahamiaji wa Kiislamu kama alivyosema awali, badala yake ametaka kufanyika uchunguzi mkali wa kuwachuja wenye msimamo mkali wanaotaka kuingia nchini Marekani. Lakini mpinzani wake Clintoni hakumwacha hata kidogo alimtuhumu moja kwa moja kwa kusema mambo mabaya na yenye kuleta mgawanyiko dhidi ya Waislamu.

Aidha aliongeza kusema imekuwa vizuri kwa mtu mwenye mhemko kama ya Donald Trump sio msimamizi wa sheria za nchini jambo ambalo lilimfanya Trump amjibu hapo hapo kwa kuwmabia "ungekuwa gerezani". Na kuendelea kumshambulia kwa kutumia barua pepe binafsi wakati akiwa waziri wa mambo ya nje 2009 hadi 2013. Jambo ambalo Clinton mara kadhaa alikiri makosa.

Mwandishi: Sudi Mnette DPA
Mhariri: Iddi Ssessanga