1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Clinton awasifu wanaharakati nchini Uganda

Sekione Kitojo4 Agosti 2012

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Hillary Clinton Ijumaa(03.08.2012) amewasifu wanaharakati waliopinga mswada wa sheria kali nchini Uganda unaowalenga mashoga, akisema wanawatia moyo watu wanaodai haki sawa.

https://p.dw.com/p/15jp1
A Ugandan man reads the headline of the Ugandan newspaper "Rolling Stone" in Kampala, Uganda. Tuesday, Oct. 19, 2010, in which the papers reveals the identity of allegedly gay members of Ugandan society and calls for public punishment against those individuals. The "Rolling Stone" is a fairly new publication under the management of Giles Muhame, a Ugandan journalist..rights activitists say that at least four homosexuals have been attacked since a Ugandan newspaper published an article this month called "100 Pictures of Uganda's Top Homos Leak _ Hang Them." A year after a Ugandan legislator tried to introduce a bill that would have called for the death penalty for being gay, rights activists say homosexuals face a host of hostility. (AP Photo)
Wanaharakati wanaopinga mswada dhidi ya mashoga nchini UgandaPicha: Katherine Fairfax Wright

Clinton ameutunukia muungano wa makundi ya haki za binadamu nchini Uganda tuzo ya wizara ya mambo ya kigeni ya mwaka 2011 ya utetezi wa haki za binadamu , ambayo ni ishara kwa mataifa ya Afrika na ya Kiislamu kuwa Marekani haitarejea nyuma katika mapambano yake dhidi ya ukandamizaji wa kisiasa na kisheria dhidi ya mashoga.

Ni muhimu kwa Waganda , serikali na raia kwa pamoja , kukemea dhidi ya ukandamizaji, unyanyasaji, pamoja na kutishwa kwa mtu yeyote. Hii ni kweli kwa mtu yeyote hata kama anatoka wapi, wanaimani gani, ama wanampenda nani, Clinton amesema.

epa02271712 Twenty seven-year-old Ugandan lesbian woman 'Biggie' (L) and her twenty four-years-old bisexual girlfriend (R) who wishes to remain anonymous for security reasons hang out at FARUG (Freedom and Roam Uganda) office in an undisclosed location on the outskirts of Kampala, Uganda's capital, 30 July 2010. Although she doesn't limit herself to lesbian relationships, Biggie's partner says she fell in love with Biggie's tenderness and the couple started dating in early 2010. FARUG, Uganda's lesbian, bisexual, transgender and intersex human rights group, has been working to push for the full equal rights of the sexual minorities and recognition of the same sex relationship in Uganda since its establishment in 2003. In October 2009, Ugandan parliamentarian David Bahati introduced a bill titled 'Anti-Homosexuality Bill' which if passed would increase and expand the penalties for already-illegal 'homosexual acts' to life imprisonment, or in some cases, the death penalty. EPA/DAI KUROKAWA
Wapenzi wa jinsia moja nchini UgandaPicha: picture-alliance/dpa

Clinton amesema kuwa amelizusha suala hilo katika mazungumzo siku ya Ijumaa na rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, ambaye serikali yake imekuwa ikishutumiwa kwa kuruhusu viongozi wa kidini na kisiasa kupigia upatu hisia dhidi ya mashoga katika nchi hiyo ya kihafidhina ya Afrika mashariki.

Mfano kwa wote

Nyie ni mfano kwa wengine na mfano kwa dunia, Clinton amewaambia wawakilishi wa kundi, lililoundwa mwaka 2009 kupambana na mswada wa sheria ambao unapendekeza adhabu ya kifo kwa yeyote atakayehukumiwa kwa kosa la ushoga.

U.S. Secretary of State Hillary Clinton speaks at the University of Dakar in Senegal, August 1, 2012. Clinton urged Africa on Wednesday to recommit to democracy, declaring the "old ways of governing" can no longer work on a continent boasting healthy economic growth and an increasingly empowered citizenry. REUTERS/Joe Penney (SENEGAL - Tags: POLITICS) // eingestellt von se
Hillary Clinton akizungumza katika ziara yake katika bara la AfrikaPicha: Reuters

Mswada huo , ambao ulizusha shutuma kali duniani, ulikwama bungeni lakini umerejeshwa tena katika umbo ambalo limetoholewa na kuwasilishwa na mwanachama wa chama cha Museveni.

President Yoweri Museveni of Uganda answers questions during a news conference following graduation ceremonies at Command and General Staff College in Fort Leavenworth, Kan., Friday, June 13, 2008. Museveni was at Fort Leavenworth to watch his son graduate. (AP Photo/Orlin Wagner)
Rais wa Uganda Yoweri MuseveniPicha: AP

Mswada huo mpya umeondoa kipengee cha adhabu ya kifo, lakini bado unalenga katika kufanya kinyume na sheria kupigania haki za mashoga, na kumuadhibu yeyote ambaye atachangia kwa fedha, kufadhili ama kusaidia ushoga.

Hatua ya Clinton ya kuonyesha mshikamano na jamii inayonyanyaswa ya mashoga nchini Uganda inakuja wakati anaendelea na ziara yake ya mataifa saba katika bara la Afrika.

Siku ya Ijumaa alifanya ziara katika taifa jipya la Sudan kusini, ambako aliitaka serikali mpya ya nchi hiyo mjini Juba kufanya makubaliano na watawala wao wa zamani Sudan ya kaskazini ili kutatua mzozo unaohusiana na mapato ya mafuta, hali ambayo imesababisha mataifa yote kuingia katika mkwamo wa kiuchumi.

Joseph Kony (* um 1961 in Odek, Uganda) ist der Anführer der Lord’s Resistance Army („Widerstandsarmee des Herrn“, LRA), einer Rebellengruppe, die die Zivilbevölkerung im Norden Ugandas und mittlerweile auch in der Zentralafrikanische Republik und Demokratischen Republik Kongo sowie Südsudan terrorisiert und der Regierung Ugandas unter Yoweri Museveni den Krieg erklärt hat, mit dem Ziel, ein theokratisches Herrschaftssystem in Uganda einzuführen, das auf den Zehn Geboten basieren soll. FILE - In this Nov. 12, 2006 file photo, the leader of the Lord's Resistance Army, Joseph Kony answers journalists' questions following a meeting with UN humanitarian chief Jan Egeland at Ri-Kwamba in southern Sudan. A video by the advocacy group Invisible Children about the atrocities carried out by jungle militia leader Joseph Kony's Lord's Resistance Army is rocketing into viral video territory and is racking up millions of page views seemingly by the hour. (Foto:Stuart Price, File, Pool/AP/dapd)
Kiongozi wa kundi la LRA Joseph KonyPicha: AP

Kony atasakwa kwa ndege

Uganda ambayo ni mshirika mkubwa wa Marekani katika masuala ya usalama , imechangia kwa kiasi kikubwa jeshi la umoja wa Afrika nchini Somalia na Clinton amesema kuwa ndege zisizo na rubani huenda zikatumika kuisaidia Marekani na Uganda katika juhudi zake za pamoja kumsaka kiongozi wa kundi la LRA Joseph Kony.

Leo Jumamosi (04.08.2012) anakwenda nchini Kenya, kabla ya kuendelea na safari hadi Malawi na Afrika kusini.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre

Mhariri : Bruce Amani.