1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Clinton akutana na Abbas

Kabogo Grace Patricia25 Septemba 2010

Mazungumzo kati ya Clinton na Abbas yalikuwa na lengo ya kuzuia mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina yasivunjike.

https://p.dw.com/p/PMVg
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton akiwa na Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas.Picha: AP

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton amekutana na Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas mjini New York kwa mazungumzo ya dharura ili kuzuia mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina yasivunjike.

Mkutano wa awali kati ya viongozi hao wawili haukuwa na matokeo mapya, lakini mkutano mwingine umepangwa kufanyika hii leo.

Muda wa kusitishwa kwa muda ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi unamalizika kesho.

Suala hilo linatishia kuyavunja mazungumzo hayo ya amani. Afisa wa Israel amesema makubaliano kuhusu ujenzi wa makaazi huenda yakafikiwa, lakini haitowezekana kusimamisha kabisa ujenzi huo.

Rais Abbas amesema atajiondoa katika mazungumzo hayo ya amani na Israel kama ujenzi huo wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi utaendelea.