1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CIZRE:Ujumbe wa Iraq kuzuru Uturuki

25 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cq

Ujumbe wa ngazi za juu wa Iraq unatarajiwa kuzuru mji wa Ankara nchini Uturuki hii leo baada ya maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Uturuki kupendekeza hatua ya kuiwekea Iraq vikwazo vya kiuchumi.Hatua hiyo inadhamiria kuilazimisha Iraq kupambana na waasi wa Kikurdi kwenye eneo la kaskazini mwa Iraq.Uturuki inafikiria hatua ya kufanya mashambulizi kwenye eneo la mpakani.Ndege za kivita za Uturuki hapo jana ziliripotiwa kutokea eneo la kusini magharibi la Diyarbakir na kushambulia kambi za waasi wa PKK kwenye eneo la mpakani.

Uturuki inatisha kufanya mashambulizi kaskazini mwa Iraq endapo Wairaqi walio na asili ya Kikurdi pamoja na majeshi ya Marekani hayatapambana na waasi wa PKK.Daniel Fried ni waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Ulaya.

''Huenda tusitarajie mafanikio kamili ila tunataka kuona asilimia mia za juhudi.Kuna mambo ambayo yanaweza kufanyika katika eneo la tukio na uongozi wa Iraq unaojali utawala ulio nao unapaswa kuchukua hatua hizo.''

Iraq kwa upande

Wake imekubali kufunga afisi za waasi hao wa PKK ila Uturuki inataka majeshi ya Marekani na Iraq kushambulia ngome za waasi hao aidha kuwarejesha viongozi wao nchini Uturuki.