1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chuma cha Rafa Benitez ki motoni?

28 Desemba 2015

Mwaka wa 2015 huenda ukamalizika vibaya kwa kocha wa Real Madrid Rafa Benitez, ambaye anaripotiwa kuwa katika hatari – hata ikiwa taishinda Real Sociedad Jumatano wiki hii au la

https://p.dw.com/p/1HUfZ
Fußball UEFA Europa League SSC Napoli - Dnjepr Dnjepropetrowsk
Picha: Getty Images/F. Pecoraro

Kocha huyo ana siku mbili tu kujua hatima yake uwanjani Estadio Santiago Bernabeu kuhusiana na uongozi wake wa miezi sita wenye misukosuko kama kocha wa Real Madrid.

Hatima ya Benitez haitategemea tu namna timu yake yenye gharama kubwa zaidi na ambayo inayumba itakavyocheza Jumanne dhidi ya Real Sociedad, lakini pia namna atakavyokaribishwa na mashabiki wasioridhishwa wa Madridista. Rais wa Real Madrid Florentino Perez anaripotiwa kusema kuwa atawasikiliza mashabiki wa Bernabeu kabla ya kuamua kama atampiga kalamu. Siku kumi zilizopita kabla ya mchuano wa nyumbani dhidi ya Rayo Vallecano, kulikuwa na sauti za kumzoea Mhispania huyo.

Uchuguzi wa maoni kupitia mitandao uliofanywa na magazeti ya michezo ya AS na Marca yanaonyesha kuwa asilimia 70 ya wasomaji wanataka Benitez aonyeshwe mlango. Kocha wa timu ya akiba Zinedine Zidane anaonekana kupigiwa upatu kuchukua nafasi yake, mbele ya Jose Mourinho.

Mwisho wa michezo kwa sasa, shukrani kwa kujiunga nami, nimekuandalia mengi kwenye ukurasa wetu wa michezo, fungua dw.com/Kiswahili, na pia wasiliana nami kwenye facebook na Twitter, mimi ni Bruce Amani. Kwaheri

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef