Imran Khan ajenga daraja kati ya mashariki na magahribi
29 Septemba 2019Alizungumzia Uislamu - dini yake - lakini alitumia rejea kama vile filamu ya Charles Bronson ya "Death Wish" na igizo la Monty Python, na marubani wa Japan wa kujitoa muhanga wa kamikaze wakati wa vita kuu vya pili vya dunia. Alijenga madaraja ya lugha na utamaduni wa kisasa wakati akijenga hoja zake kwa umakini mkubwa.
Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan, alitumia ustadi kuelezea chapa yake yake ya "mashariki inakutana na magharibi" kwenye jukwaa la Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa, akijaribu kufafanua hatari ya chuki dhidi ya Uinslamu na kwa nini Waislamu wanaguswa hasa na mashamblizi dhidi ya Mtume Muhammad (SAW).
Mwishowe, hotuba ya Khan ilifikia kituo chake - shambulio la kisiasa kutoka kwa mwanasiasa dhidi ya ukandamizaji wa India katika eneo la Waislamu wengi la Kashmir. Ingawa njiani, alitoa mwito uliozoeleka na Waislamu wengi lakini ambao kwa namna fulani haukuwa wa kawaida katika jukwaa la kimataifa: Utetezi kamili wa Uislamu ulioandaliwa kwa ajili ya masikio ya hadhira ya Kimagharibi.
"Ni muhimu kuelewa hili. Mtume (Muhammad) anaishi katika nyoyo zetu," Khan alisema. "Anapodhihakiwa, anapotukanwa, inauma."
"Sisi wanadamu tunafahamu kitu kimoja: Maumivu ya moyo yanauma zaidi kuliko maumivu ya kimwili," alisema katika hotuba yake iliyozunguka kati ya utambulisho wake wa aina mbili - nyota wa michezo na jukumu lake la sasa kama kiongozi wa taifa kubwa zaidi duniani la Kiislamu.
Ufahamu wake wa fikra za magharibi
Sawa na maisha yake, ambayo kwa sehemu kubwa yamekuwa kwenye magazeti ya udaku katika miaka ya 1990, hotuba ya Khan iliyodumu kwa dakika 45 ilionekana kufuata siyo maandishi lakini mtiririko wa ufahamu wake usiyo wa maandalizi.
Hata kama mjumbe alikuwa wa kisiasa zaidi, ujumbe wake ulikuwa wa kiutu zaidi. Ulisema kimsingi, kwamba ugaidi, itikadi kali na mashambulizi ya bomu ya kujitoa muhanga siyo sehemu ya dini yoyote - au angalau havipo katika dini moja tu.
Wakati wa Vita kuu vya Pili vya Dunia, Khan alisema, Japan ilitumia marubani wa kamikaze kama waripuaji wa kujitoa muhanga. "Hakuna alielaumu dini." Lakini baada ya mashambulizi ya 9/11, Waislamu wa dunia - na hasa wa kutoka Pakistan na mataifa mengine machache - walijikuta wakilaumiwa kutokana na matendo ya watekaji wa ndege waliolenga makao makuu ya shirika la biashara duniani WTO, wizara ya ulinzi Pentagon na ndege ya abiria yenye nambari ya Safari 93.
"Mashambulizi ya kujitoa muhanga yalilinganishwa na Uislamu," alisema. Alisema Viongozi wa Kiislamu walishindwa baada ya mashambulizi ya 9/11 kuelezea kwama "hakuna dini inayohubiri itikadi kali." Badala yake, alisema, viongozi wa Kiislamu walianza kuva suti za magharibi, na hata wale wasiojua Kiingereza walianza kuzungumza Kiingereza "kwa sababu walikuwa wanafuata msimamo wa wastani."
Wakiwa na hofu kubwa ya kupachikwa jina la itikadi kali, viongozi wa Kiislamu waligeuka wa kati kuliko kusimama imara katika kusema "hakuna kitu kama Uislamu wa itikadi kali," alisisitiza.
Akili za magharibi kuhusu Uislamu
Wakati Khan akisimama mbele ya viongozi wa dunia, mwenyewe akiwa moja wao, alisema kwamba anajua "namna akili za magharibi zinavyofanya kazi na namna watu wa magharibi wanavyoitazama dini." Alizungumza kama Muislamu wa Pakistan - alielowea katika utamaduni wa magharibi, watoto wake wakiwa nusu Waingereza - aliemuoa kiongozi wake wa kiroho na ambaye amekuwa waziri mkuu.
Khan alisema anafahamu kwa nini "mtu mjini New York, maeneo ya Midwest nchini Marekani, katika mji mkuu wa nchi ya Ulaya" anaweza kufananisha Uislamu na itikadi kali na kushangazwa na hisia za hamaki za Waislamu dhidi ya kudhihakiwa Mtuma Muhammad (SAW).
Alikumbuka kwa mshangao, mara ya kwanza alipokwenda England na kusikia kuhusu filamu iliyokejeli maisha ya Yesu Kristu - akimaanisha tamthilia ya vichekesho ya mwaka 1979 ya "Monty Python's Life of Brian," iliyopendwa na Waingereza wengi pamoja na Wamarekani.
"Ni jambo lisiloweza kufikirikika katika jamii za Waislamu," alisema kuhusu kumdhihaki mtume yeyote. Baadhi katika mataifa ya magharibi waliofanya hivyo wamelengwa na washambuliaji wa Kiislamu, maarufu zaidi likiwa gazeti la vikaragosi la Charlie Hebdo la nchini Ufaransa.
Katika maneno ya Khan, inategemea kiwango cha hisia - na kuwa na hisia juu ya kile kinachosababisha maumivu kwa binadamu wengine." Ili kufikisha ujumbe wake, alitoa mfano wa mmoja ya masuala nyeti zaidi kwa mataifa ya magharibi, akisema mauaji ya Wayahudi (Holocaust) yanachukuliwa "kwa usahihi" na hisia za juu kwa sababu yanasababisha maumivu kwa jamii ya Wayahudi.
"Msitumie uhuru wa kujieleza kusababisha maumivu kwetu kwa kumtukana mtume wetu. Hicho tu ndiyo tunataka," alisema.
Wakosoaji wa Khan
Nyuma ya maneno yake ya kuisogeza dunia, Khan alieingia madarakani mwaka uliyopita, hajakosa wakosoaji. Wanasema yeye - sambamba na jeshi la Pakistan na idara ya upelelezi hasa - wametoa nafasi kwa wale wanaokumbatia vurugu, na kuondoa nafasi kwa watu nchini mwake, wanaotaka taifa la kidemokrasia, na siyo mfumo wa kidini.
Khan amezungumza kutetea jamii za wachache. Ingawa bado hajachukuwa msimamo thabiti au kuunga mkono wale wanaotaka kupunguza makali baadhi ya sheria za Pakistan - zikiwemo zinazohusu kukufuru dini ambayo inatoa adhabu ya kifo kwa wale wanaoudhalilisha Uislamu.
Kama kiongozi mpya, hotuba ya Ijumaa ndiyo ilikuwa ya kwanza kwake mbele ya baraza la Umoja wa Mataifa na kwa njia hii ya hadhira ya kimataifa, aliifanya kuwa na athari chanya. Aliitolea mwito kanda ya Ghuba kuwa kamusi ya tafsiri kwa ajili ya tamaduni mbili zinazojikuta katika msuguano.
Mwanasia ndani ya Khan
Kwa muda mrefu mitizamo mingi zaidi ya magharibi kuhusu ulimwengu wa Kiislamu ilikuwa mipana na hata ya istihizai. Hebu fikiria mfano wa "Aladdin" au Ali Baba" - kutoka waliopotoshwa hadi matusi ya waziwazi. Lakini duniani, kilichokuzwa zaidi ulikuwa mtizamo wa magharibi. Ijumaa Khan alipata fursa ya kubadili mambo kidogo.
Mwanasiasa ndani ya Khan alifanya kile kilichotarajiwa wakati wa hotuba yake: Alitumia jukwaa lake kuhamia kwenye kuionya India kuhusiana na sera zake kuelekea jimbo la Kashmir.
Lakini katika kusimama mbele ya hadahra ya Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa akiwa na mguu katika dunia mbili, pia aliibua maswali ambayo ni muhimu zaidi kwa wakati huu wa safari ya mwanadamu. Wengi wetu hivi sasa tuna uhakika namna tunavyohisi kuhusu wale ambao ni tofauti na sisi.
Ujumbe kutoka Ijumaa - iwe ulikusudiwa au la - ni kwamba maumivu na kakara vinaweza kuwa vya dunia nzima, lakini wafasiri wapo karibu.
chanzo: ape