1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yawafundisha Waighuru propaganda kambini kwa lazima

Saumu Mwasimba Mhariri: Iddi Sessanga
8 Juni 2020

Mateso na unyanyasaji wa kutisha vimeripotiwa katika makambi ya kutoa elimu kwa watu wanaoshikiliwa katika vituo maalum kwenye mkoa wa Xinjiang. Watu wanafundishwa kwa lazima elimu ya propaganda.

https://p.dw.com/p/3dSBX
China | Muslime | Umerziehungslager
Picha: Getty Images/AFP/G. Baker

Makambi hayo ya serikali ya China imeripotiwa watu wanaoshikiliwa huko wanalazimishwa kukaa saa chungu nzima katika darasa wakofunzwa elimu ya propaganda kuelekea China na lugha huku wakiwa wamekalia viti vidogo. Katika baadhi ya vituo hivyo wanalazimika kutazama vipindi virefu vya Propaganda kwenye televisheni vilivyomsifia rais Xi Jinping. Ripoti ifuatayo inatowa taswira ya makambi hayo kupitia maelezo yaliyotolewa na waliowahi kufungwa kwenye vituo hivyo.

Imeripotiwa kwamba ndani ya makambi hayo mtu anapojaribu kuzungumza na mwenzie hata kwa sauti ya kunong'onezana adhabu kali ilitolewa kwa watu hao.

Lakini hata baada ya kukaa kwa miezi chungunzima kwenye vizuizi hivyo baadhi ya waliowahi kufungwa huko wanaripoti kwamba siku moja hali ilibadilika na kuwa tofauti.

Wanasema walikabidhiwa orodha ndefu ya makosa,na wafungwa wote walitakiwa kuchagua kila mmoja uhalifu uliomfanya afungwe,wakati mwingine kwa miezi kadhaa na mara nyingine bila hata ya kuambiwa kwanini hasa walikamatwa.

Baada ya kuchagua uhalifu kwenye orodha waliyopewa ilifuatia kesi ya magumashi au kesi ya kiini macho ambayo wafungwa hawakuwa na uwakilishi wa aina yoyote wa kisheria na walishtakiwa na kuhukumiwa bila ya kuwepo ushahidi au kufanyika mchakato wowote ule.

Dw ilizungumza na wafungwa wanne wa zamani wanaume wawili na wanawake wawili kutoka Xijiang,eneo ambalo ni la vijijini kabisa huko Kaskazini Magharbi mwa China, ambako idadi kubwa ya wakaazi ambao ni waislamu wamekuwa kwa kipindi kirefu wakilabiliwa na ukandamizaji unaofanywa na maafisa wa utawala wa China, ikiwemo katika miaka ya karibuni kuwafunga kwa kipindi kirefu kwenye makambi maalum a mafunzo.

Wafungwa wote hao wazamani waliwahi kukaa kwa miezi kadhaa jela Xinjiang katika mwaka 2017 na 2018.

Imeripotiwa kwamba ndani ya makambi hayo mtu anapojaribu kuzungumza na mwenzie hata kwa sauti ya kunong'onezana adhabu kali ilitolewa kwa watu hao.
Imeripotiwa kwamba ndani ya makambi hayo mtu anapojaribu kuzungumza na mwenzie hata kwa sauti ya kunong'onezana adhabu kali ilitolewa kwa watu hao.Picha: Reuters/T. Peter

Wafungwa walazimishwa kujichagulia mashtaka dhidi yao

Kila mmoja alionekana kuikumbuka siku waliyopewa kikaratasi kilichokuwa kimeandikwa mashtaka zaidi ya 70 na kulazimishwa kila mtu kuchagua shtaka moja kati ya mengi yaliyoorodheswa.

Baadhi ya mashtaka hayo yalionekana kama hayana madhara makubwa kama kusafiri au kuwasiliana na watu wanaokaa nje ya nchi.

Lakini mengi yalihusiana na dini kwa mfano kuswali au kuvaa mitandio ya kichwa. Hata hivyo wafungwa hao wanne wa zamani walifanikiwa kuhamia katika nchi jirani ya Kazakhstan kufuatia shinikizo la umma kutoka kwa wanafamilia wanaoishi huko na pengine zaidi ni kutokana na juhudi za kidiplomasia za nyuma ya pazia zilizofanywa na serikali ya Kazakhstan.

Kufuatia hali hiyo serikali ya China iliwaachia huru wale waliokuwa na vibali vya ukaazi wa Kazakhstan,hati za kusafiri na waliokuwa na jamaa zao wanaoishi Kazakhstan ambako ni nyumbani kwa jamii kubwa kiasi ya Waiguru.

Kadhalika imeripotiwa kwamba ni vigumu sana kwa wale wasiokuwa na uhusiano na uraia wa nje kufanikiwa kuepuka mtandao mkubwa wa ukandamizaji wa China na kufuatiliwa kila wakati.

Wakati DW haiwezi kuthibitisha ukweli juu ya kilichoelezwa na wafungwa hao wanne wa zamani,maelezo yao yanawiana katika mambo muhimu. Kila mmoja amesimulia alivyopewa orodha ya kuchagua kwa lazima uhalifu uliofanya ajikute mfungwa. Tangu mwaka 2016 serikali ya China imekuwa ikiwakamata watu wa jamii ya Waiguru na Wakazakhstan na kuwafunga katika kile kinachoitwa na China kama vituo vya mafunzo ya muda lakini nchi za Magharibi vinasema ni makambi ya kuwabadilisha watu mtazamo wa imani zao. Ni vigumu kusema hasa ni watu wangapi wamefungwa kwenye kambi hizo za China.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW