1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yatetea hatua ya kutoa zawadi kukamatwa kwa wapinzani

16 Desemba 2023

China imetetea hatua yake ya kutoa zawadi ya dola 128,000 ili kupata taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa wapinzani wa Hong Kong waliotorokea ng'ambo

https://p.dw.com/p/4aFfX
Picha za wanaharakati watano wanaosakwa na serikali ya China zilizotolewa Desemba 14,2023
Picha za wanaharakati watano wanaosakwa na serikali ya ChinaPicha: Tyrone Siu/REUTERS

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Mao Ning, amesema China imekataa ukosoaji huo wa nje na kusema maagizo ya kukamtwa kwa watu hao yalihitajika na ni ya haki kulingana na sheria na utaratibu wa kimataifa.

Soma pia:Polisi ya Hong Kong yatoa zawadi ya pesa kwa habari kuhusu wanaharakati watano walioko Marekani

Bila ya kutaja moja kwa moja zawadi hiyo ya pesa, Mao amesema mataifa mengine yana vipengee vingine kwa sheria zao kuhusu usalama wa kitaifa na kuongeza kuwa uungaji mkono wa serikali za nje kwa walio orodheshwa ni kuficha lengo lao la kuiyumbisha Hong Kong.

Wakati wa mkutano wa kila siku na wanahabari, Mao amewaambia kwamba wanapinga vikali na kudharau nchi zinazokosoa sheria ya usalama wa kitaifa ya Hon Kong na kuingilia mifumo ya mahakama.