1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaChina

China yafafanua chanzo cha ongezeko la magonjwa ya kupumua

26 Novemba 2023

Wizara ya afya ya China imesema hii leo kwamba, ongezeko la magonjwa ya kupumua nchini China humo yanatokana na mafua na vimelea vingine vinavyojulikana na sio kutokana na virusi aina ya Novel

https://p.dw.com/p/4ZSXY
Watoto na wazazi wao wasubiri matibabu nje ya hospitali moja mjini Beijing mnamo Novemba 23,2023
Watoto na wazazi wao wasubiri matibabu nje ya hospitali moja mjini BeijingPicha: Jade Gao/AFP

Wizara hiyo imezitaka mamlaka za miji nchini humo kufungua kliniki zaidi za homa na kuhamasisha kuhusu chanjo miongoni mwa watoto na wazee wakati taifa hilo likikabiliana na wimbi la magonjwa ya kupumua wakati wa msimu wa baridi kali tangu kuondolewa kwa vizuizi vya janga la Uviko-19.

Soma pia:WHO: China watoe data ya ongezeko la maradhi ya kupumua

Msemaji wa wizara hiyo Mi Feng, amesema juhudi zinapaswa kuimarishwa kuongeza kliniki husika na maeneo ya matibabu, kuongeza saa za huduma na usambazaji dawa.

Mapema wiki hii, shirika la afya ulimwenguni WHO liliitaka China kutoa maelezo zaidi juu ya maradhi hayo ya kupumua miongoni mwa watoto yaliyozua wasiwasi, kufuatia ripoti kadhaa za vyombo vya habari na mashirika yanayofuatilia magonjwa ya kuambukiza duniani.