SiasaChina
China yasema msimamo wake haujabadilika kuhusu Rasi ya Korea
20 Februari 2023Matangazo
Kauli hiyo imetolewa leo na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin, baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora ya masafa mafupi mapema leo asubuhi.
Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili katika pwani yake ya mashariki, huku Kim Yo Jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, mwenye nguvu na ushawishi mkubwa, akisema kuwa hatua ya Korea Kaskazini kuitumia Bahari ya Pasifiki kama eneo lake la kufyatua makombora, itategemea tabia ya vikosi vya Marekani.
Wakati huo huo, Japan imetoa ombi la kufanyika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya Korea Kaskazini kufyatua makombora hayo.