China yaongeza bajeti yake ya kijeshi.
6 Machi 2004Matangazo
BEIJING: Jamhuri ya Umma wa Uchina mwaka huu inataka kuongeza bajeti yake ya kijeshi kwa asili miya 11.6 na kutumia EURO biliyoni 2.1 zaidi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya bajeti iliyokabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Fedha Jin Renqing mbele ya bunge linalokutana mjini Beijing. Pia Waziri huyo alitangaza kuwa bajeti itaongezwa kwa asili miya 20 nyingine kwa shabaha ya kunyanyua hali za wakulima. Mkuu wa Halmashauri ya Marekibisho, Mai Kai alisisitiza kuwa Uchina itaendelea kudumisha thamani tulivu ya sarafu yake Yuan kulinganishwa na Dollar ya Kimarekani.