China yaongeza bajeti yake ya kijeshi.
6 Machi 2004Matangazo
BEIJING: Jamhuri ya Umma wa Uchina mwaka huu inataka kuongeza bajeti yake ya kijeshi kwa asili miya 11.6 na kutumia EURO biliyoni 2.1 ziada. Mwongezeko huo ni mara dufu kupita mwongezeko wastani wa bajeti nzima. Akitangaza hayo mbele ya bunge linalokutana mjini Beijing, Waziri wa Mambo ya Fedha Jin Renqing alikisoa pia siasa ya Taiwan. Lakini badala ya kutoa tamshi la kuionya Taiwan, katika hutuba yake Waziri wa Mambo ya Nje Li Zhaoxing alisisitiza mahusiano ya watu wa nchi hizo mbili. - Baada ya kukabiliana na muflisi wa EURO biliyoni 31 katika miaka ya karibuni, kwa mara ya kwanza kasoro hiyo ya bajeti ya Uchina haijaongezeka mwaka huu. Lakini kimerudi nyuma kiwango cha ustawi wake wa kiuchumi ambacho mwaka uliopita kilifikisha asili miya 9.1.