China yakumbwa na mashambulizi ya mtandaoni
23 Septemba 2024Kwa mujibu wa wizara hiyo iliyotolewa leo, mashambulizi hayo yanasambaza ujumbe unaokashifu viongozi na mfumo wa kisiasa wa China Bara na sera za kimsingi za taifa hilo la kikomunisti.
Wizara hiyo imewataka raia kuripoti matukio yoyote yanayojiri kwenye vifaa vyao ya kieletroniki kuhusiana na mashambulizi hayo.
Soma zaidi: Waziri wa Ulinzi China ahimiza mataifa makubwa kuongoza juhudi za amani duniani
Mara kadhaa, watumiaji wa simu za mkononi, kompyuta ama televisheni hutumiwa ujumbe kwenye vifaa vyao wenye picha na maelezo ya kumlaani Rais Xi Jinping.
China inaamini kuwa kundi hilo la wadukuzi lina makao yake nchini Taiwan.
Taiwan yenyewe imekuwa ikisema kuwa makundi ya wadukuzi wa China yamekuwa yakisambaza taarifa za uongo kwenye kisiwa hicho kinachojitawala chenyewe.