1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yakosoa vizuizi vya UVIKO dhidi ya raia wake

4 Januari 2023

Serikali ya China imekosoa vikali masharti ambayo yamewekwa na mataifa kadhaa dhidi ya wasafiri kutoka nchi hiyo, ya kuwataka wafanye vipimo vya maambukizi ya virusi vya korona.

https://p.dw.com/p/4Litw
BG China Coronavirus | Bahnhof in Wuhan
Picha: Tingshu Wang/REUTERS

China imetishia kuchukua hatua za kukabiliana na nchi zinazohusika ikiwemo Marekani na nyingine kadhaa za Ulaya.

Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, alisema jana Jumanne kwamba wanaamini masharti ambayo baadhi ya nchi zimeweka yanailenga China ilhali hayana msingi wowote wa kisayansi na baadhi yao hayakubaliki.

Kufuatia ongezeko la visa vya maambukizi ya UVIKO-19 nchini China, Australia na Canada zilijiunga na nchi nyingine kama Marekani, India, Japan, Korea Kusini na nyingine kadhaa za Ulaya ambazo zinawataka wasafiri kutoka China kufanya vipimo kabla ya kuanza safari zao.

Umoja wa Ulaya nao unatarajia hivi leo kutangaza utaratibu utakaozingatiwa kote Ulaya kuhusiana na abiria kutoka China.