1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yakabiliwa na hali ya hewa mbaya kuwahi kutokea nchini humo

29 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CzM7

BEIJING:

China inakabiliwa na majira ya baridi makali kuwahi kutokea nchini humo kwa kipinda cha miongo mitano. Hali hiyo inaongezeka kuwa mbaya na kusababisha hasara.Theruji imesababisha kukatika kwa umeme katika miji mingi nchini humo na usafiri umeathirika mno. Safari kadhaa za reli pamoja na ndege zimefutwa na hivyo kuvuruga mipango ya safari ya mamilioni ya waChina ambao walikuwa wanapanga kwenda nyumbani kusherehekea mwaka wao mpya ambao unaanza wiki ijayo.Inasemekana watu wanaofikia 50 wameuawa na hali hii .Takriban mabasi mawili yaliacha njia baada ya kutereza kwenye theruji na kuwauwa watu 25 katika tukio moja.Na katika tukio lingine watu wanne ndio walipoteza maisha yao. Hali hii ya hewa inalikabili eneo la kusini la China kutoka mkoa wa Xinjiang kaskazini magharibi hadi Fujiani kusini mashariki.