1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yadai ´kupakwa tope´ kupitia hotuba ya Biden

8 Februari 2023

China imesema imechafuliwa jina katika hotuba ya Rais wa Marekani Joe Biden ya Hali ya Taifa ambayo ilitaja mara kadhaa ushindani kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4NFeM
USA Washington | State of the Union | Joe Biden
Picha: Jacquelyn Martin/AFP/Getty Images

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya China Mao Ning amesema China haiogopi kushindana na Marekani lakini inapinga kubainishwa kwa uhusiano mzima wa China na Marekani kwa misingi ya ushindani.

Mao amesema China itayalinda maslahi yake na Marekani inapaswa kushirikiana nayo ili kuhimiza kurejea kwa mahusiano ya pande zote kwenye mkondo sahihi na wenye maendeleo imara.

Biden aliitaja China na kiongozi wake Ji Xiping karibu mara saba katika hotuba yake ya jana usiku, akilenga hasa kuhusu jinsi Marekani inavyoendelea kujiandaa kushindana na Beijing wakati pia akilenga kuepusha mzozo.