1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaonya kuanzishwa ushirika wa kijeshi Asia-Pasifiki

Hawa Bihoga
4 Juni 2023

Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu ametahadharisha juu ya kuanzishwa ushirika wa kijeshi kama ule wa NATO katika eneo la Asia -Pasifiki, akisema kwamba hatua kama hiyo italitumbukiza eneo hilo katika migogoro.

https://p.dw.com/p/4SAgh
Singapur Shangri La Dialog | Li Shangfu
Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Li ameyasema hayo katika mkutano wa Usalama wa Singapore ikiwa ni siku moja baada ya meli za kijeshi za Marekani na China kusafiri hadi karibu na mlango wa bahari wa Taiwantukio ambalo limeibua hasira kutoka pande zote.

Katika mkutano huo ambao pia unahudhuriwa na waziri wa Ulinzi Marekani  Lloyd Austin, Li ameionesha Marekani kama sababu ya kukosekana kwa utulivu wa kikanda, na China kama inataka kupunguza hali ya mvutano.

Soma pia:Marekani yasema mazungumzo na china ni muhimu ili kuepuka Mzozo

Hapo jana waziri  Lloyd Austin alihimiza juu ya mazungumzo na Beijing ili kuondoa mivutano ambayo inashuhudiwa kwa hivi sasa.