SiasaChina
China na Korea Kaskazini waahidi kuimarisha uhusiano
6 Oktoba 2024Matangazo
Katika hotuba ya rais Rais Xi Jinping wa China kuelekea kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, Xi amesema China iko tayari kuendelea "kufungua ukurasa mpya" katika mahusiano baina ya nchi hizo kupitia mawasiliano yaliyoimarishwa na ushirikiano.
Soma pia: Korea kaskazini na China zakubaliana kulinda maslahi ya pamoja
Katika ujumbe wake kwa Xi, Kim ameahidi kujitahidi kwa kasi kuimarisha na kuendeleza mahusiano ya kirafiki na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili ili kufikia enzi mpya.
China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Korea Kaskazini. Lakini China ilijizuia kidogo mnamo mwezi Juni wakati Kim aliposaini mkataba wa kimkakati na Urusi uliohusisha pia vipengee vya ulinzi.