SiasaChina
China: Meli ya kivita ya Marekani imevuka mipaka yake
23 Machi 2023Matangazo
Taarifa ya jeshi la China imesema meli ya Marekani yenye mfumo wa kuharibu makombora aina ya USS Millus iliyoingia katika eneo la bahari la mipaka ya China inadhoofisha amani na utulivu katika njia ya maji yenye shughuli nyingi.
Lakini kwa upande wake jeshi la wanamaji la Marekani limetoa kauli ya kupinga taarifa ya jeshi la China kwa kusema meli hiyo imekuwa ikifanya opereshini za kawaida katika eneo la Bahari ya China Kusini na haikufurushwa.