1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China kuvuna medali nyingi za dhahabu katika michezo ya Olimpiki.

4 Agosti 2008

Wenyeji China huenda wakavuna medali nyingi katika mashindano yajayo ya Olimpiki , lakini Marekani itaweza kurejesha nguvu yake ya kutawala michezo hiyo katika msimamo wa medali.

https://p.dw.com/p/EqOc
Wanamichezo wa Ujerumani Lars na Barbbara Barth wakijitayarisha kwa sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo ya Olimpiki inayofanyika nchini China kuanzia tarehe 8-24 mwezi huu.Picha: congaz

Wenyeji China huenda wakashinda medali nyingi katika mashindano yajayo ya Olimpiki lakini Marekani itaweza kurejesha nguvu yake ya kutamalaki katika msimamo wa medali.

Katika utabiri wake mashuhuri unaotolewa kila mara kabla ya michezo ya Olimpiki , jarida la Amerikan magazine Sports Illustrated SI, limetabiri kuwa muogeleaji wa Marekani Michael Phelps ataweka historia kwa kuvuna medali nane za dhahabu na mwenzake Tyson Gay atamshinda mpinzani wake Mjamaika katika mbio za mita 100.

Bingwa wa China Liu Xiang anatarajiwa kushindwa na bingwa wa Cuba anayeshikilia rekodi ya dunia Dayron Robles katika mbio za mita 110 kuruka viunzi lakini hatoweza kuzuwia China kuweza kuvuna medali nyingi za dhahabu kwa mara ya kwanza.

Jarida hilo limetabiri kuwa China itamaliza ikiwa na medali 49 za dhahabu 28 za fedha na 25 za shaba na kupata medali 102 kwa jumla, wakati Marekani bado ikiwa juu kwa medali 121, ikiwa ni 44 za dhahabu, 44 za fedha na 32 za shaba. Urusi inatabiriwa kushika nafasi ya tatu kwa kupata medali 25 za dhahabu, 28 za fedha na 22 za shaba , jumla ikiondoka na medali 75.

Idadi ya mwaka 2004 ilikuwa Marekani ilipata medali 36 za dhahabu, 39 za fedha na 27 za shaba, China ilipata medali 32 za dhahabu, 17 za fedha na 14 za shaba juma medali 63 na Urusi ilipata medali 27 za dhahabu, 27 za fedha na 38 za shaba , jumla ikiwa medali 92.

China ina matumaini makubwa katika kutawala michezo hiyo inayofanyika nchini humo kuanzia August 8 hadi 24 na rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Jacques Rogge amekiri kuwa timu ya wenyeji kwa kawaida inashinda medali nyingi kuliko kawaida. Phelps mwenye umri wa miaka 23 yuko katika ukingo wa kuingia katika historia ya olimpiki isiyosahaulika, kwa mujibu wa jarida hilo la SI.

Hatarajiwi tu kuifanyia mabadiliko rekodi aliyoweka Mark Spitz ya mwaka 1972 ya medali saba za dhahabu katika michezo ya olimpiki ya wakati mmoja lakini medali zake nane kutokana na michezo tofauti mitano pamoja na mbio tatu za kuogelea pia zitamfanya kuwa mwanamichezo bora aliyewahi kupata tuzo hizo kuliko mwingine yeyote kwa kuwa na medali 14 za dhahabu na mbili za shaba.

Wanamichezo wane kwa hivi sasa wanashirikiana rekodi ya medali tisa na mwanamichezo wa Urusi anayeshiriki michezo ya ndani ya gymnastic Larisa Latynina akiwa na medali tisa za dhahabu, tano za fedha na 4 za shaba kutoka mwaka 1956 hadi 1964.

Utabiri mwingine ni kwamba bingwa wa dunia Gay atainyima Jamaika medali yake ya kwanza ya dhahabu katika mbio za mita 100 kwa kumshinda anayeshikilia rekodi ya dunia Usain Bolt, kwa kuwa mkimbiaji mwingine mwenye kasi katika mbio hizo nae akiwa Mjamaika Asafa Powel hatashiriki.

Keron Stewart ataipatia Jamaica medali ya dhahabu kwa wanawake , Muingereza Paula Darcliffe hatashiriki katika mbio za marathon, wakati Kenya itapata hatimaye medali yake ya kwanza ya dhahabu katika mbio za marathon kwa wanaume kupitia Martin Lel.

Roger Federer atafidia kupoteza nafasi yake ya namba moja katika michezo ya tennis duniani kwa kupata medali ya dhahabu hatimaye na timu ya wanaume ya mpira wa kikapu watajisafisha kwa kuumbuliwa katika michezo ya 2004 kwa kupata medali ya dhahabu safari hii. Lakini Brazil itakosa tena medali ya dhahabu katika soka, na kupoteza mchezo wake wa fainali na Argentina.

Osmay Acosta ataiongoza Cuba kupata medali tatu za dhahabu katika ngumi. Mjerumani Sascha Klein atainyima nafasi China kuzoa medali nane katika kupiga mbizi kuogelea kwa upande wa wanaume, lakini wenyeji watapata medali zote nne katika mpira wa mezani pamoja na medali sita za dhahabu katika mchezo wa badminton.

Muda wa medali ya kwanza ya dhahabu kukabidhiwa Jumamosi ijayo utakwenda kwa Mjerumani Sonja Pfeilschifter katika kulenga shabaha kwa bunduki, iwapo utabiri uliotolewa na jarida la Sports Illustrated utakuwa sahihi.